Msanii Holyman - Promise lyrics | LyricsFreak
Correct  |  Mail  |  Print  |  Vote

Promise Lyrics

Msanii Holyman – Promise Lyrics

Niliskiza redi, nikajitizama huko ndani
Kulikuwa na guitars, nyatiti pia nadhani
Na nilishaa gaagaa matiti ya mama zamani
Kama huelewi, hautakuwa na imani
Tuko engaged kaa simu, bado ako zile za tease me
Sijui kiss me, wengine sijui chips me
Sacrifice nimemake hata nimepea industry kidneys
Nakamua kaa farmer, saa zingine kaa kidis
Kanyari mbegu pesa ngapi, nipande family tree
Haujaskia the best things in life are free
Nilijua nikitoa kamasi kwa pua nikiwa class three
Yuko wapi Frash na Chris tudandie mathree
Sababu mende akitaka kurule over the kuku
Lazima amueke mwewe kaa bodyguard
Amlipe zaidi ya bugu
Lazima mawe ziwe tatu ndio tupike ugali kuni
Mguu mbili mkono mbili, vidole bado ni kumi
Unavuka fence tunadigital migrate
Tune in cheza kati you can’t cut me
Shake me, ruka bladder
Natema sana naskia kanjo wako rada
Mistari excess, nafuatwa na mamistress
Juu narun town kaa Kidesh
Unataka slap, kam na Shebesh
But simu nilipokea, ilibidi ninunue suti
I mean si tulikuja baby shower miaka tu ya juzi
Mama alimpenda lakini asubuhi hakuamka
Na vile alituacha, mama hangetamka
Alifunga ulimi four days, alitunda tumbo four days
Alikonda aisee, uchungu wa mwana
Alijua maana, aliombea manna
From fluent akaanza kustammer
After siku nne, mwana atazama
Pastor alisoma stanza, kitabu ni ya kwanza
In the beginning there was the word, then mwangaza
Mama alijaribu kujikaza, ikafika part ya mchanga
Kwa nini mtoto, na alikuwa tu mchanga
Kwa nini
Share lyrics
×

Promise comments